DARAJA kwa sasa iko kwenye awamu ya majaribio na matumizi ya awali. Wakati tunajiandaa kuizindua rasmi kwenye Google Play Store na Apple App Store, programu ya DARAJA inapatikana kupakuliwa moja kwa moja kupitia tovuti yetu.

Mwongozo huu utakusaidia ku-install programu ya DARAJA kwa usalama kwenye simu yako ya Android.


Hatua ya 1 – Pakua Programu ya DARAJA

Tembelea tovuti ya DARAJA na bonyeza button ya kupakua Programu ya DARAJA. Hii itapakua faili ya APK kwenye simu yako.
Or click this link to initiate the download.

Faili ya APK ni faili rasmi ya kusakinisha programu ya DARAJA kwenye Android.


Hatua ya 2 – Ruhusu Usakinishaji wa Programu

Kwa kuwa DARAJA bado haipo kwenye Play Store, Android itakuomba ruhusa ya kusakinisha programu kutoka nje ya Play Store.

  1. Baada ya kupakua, bonyeza faili ya DARAJA.apk
  2. Ujumbe utaonekana ukisema “For your security, your phone is not allowed to install unknown apps from this source.”
  3. Bonyeza Settings
  4. Bonyeza Allow from this source
  5. Rudi nyuma kisha bonyeza Install

Hatua hii inahitajika mara moja tu. Hakuna haja yakufanya hivi tena baada ya kufanya mara moja.


Hatua ya 3 – Install Programu

Baada ya kubonyeza install Installprogramu ya DARAJA itasakinishwa kwenye simu yako.

Usakinishaji ukikamilika:

  • Bonyeza Fungua kaunza kutumia
  • Au tafuta DARAJA kwenye orodha ya programu zako

Je, Hii Ni Salama?

Ndiyo. Programu ya DARAJA unayopakua kutoka kwenye tovuti yetu ni toleo rasmi na lililothibitishwa lililotengenezwa na timu ya DARAJA Climate Services pamoja na Centre for Community Initiatives (CCI).


Kwa Nini DARAJA Bado Haipo Kwenye Play Store?

DARAJA kwa sasa inatumika kwenye miradi ya majaribio na kwa washirika wetu ili kuboresha huduma na kuhakikisha mfumo unafanya kazi vizuri kwa wakulima, wavuvi na jamii za mijini.

Baada ya majaribio kukamilika, DARAJA itapatikana rasmi kwenye:

  • Google Play Store
  • Apple App Store

Kwa sasa, kupakua kupitia tovuti yetu kunakupa upatikanaji wa mapema wa huduma za DARAJA.


Unahitaji Msaada?

Ikiwa una changamoto yoyote ya kusakinisha au kutumia programu, tafadhali wasiliana nasi kupitia tovuti ya DARAJA au njia zetu za mawasiliano. Pia unaweza kutumia barua pepe kwenda darajaservicesapp@gmail.com.

Tuko hapa kukusaidia.

Leave a Reply

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *